Genesis 22:20-23

Wana Wa Nahori

20 aBaada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 21 bUsi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 22 cKesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 23 dBethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane.
Copyright information for SwhNEN